18 Aprili 2025 - 20:55
Source: Parstoday
Kiongozi Muadhamu: Uhusiano baina ya Iran na Saudi Arabia utafaidisha pande mbili

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesisitiza kuwa: Uhusiano kati ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Saudi Arabia utakuwa na faida kwa pande mbili na unaweza kuzifanya pande mbili hizo zikamilishane.

Ayatullah Sayyid Ali Khamenei ameyasema hayo jana Alhamisi jioni jijini Tehran alipokutana na Waziri wa Ulinzi wa Saudi Arabia, Mwanamfalme Khalid bin Salman, ambaye ni kaka wa Mrithi wa Ufalme wa Saudia Mohammed bin Salman.  Katika kikao hicho Khalid bin Salman alimkabidhi Ayatullah Khamenei barua rasmi kutoka kwa Mfalme Salman wa Saudi Arabia.

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesisitiza katika ikao hicho kuwa: Tunaamini uhusiano kati ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Saudi Arabia utakuwa wa manufaa kwa nchi zote mbili, na pande mbili zinaweza kukamilishana." Akisisitiza kwamba kuna pande zisizopenda kuona uhusiano kati ya nchi hizi mbili ukipanuka zaidi, Ayatullah Khamenei amesema: "Nia hizi za uhasama lazima zishindwe, na sisi tuko tayari kwa jambo hili." 

Imam Khamenei ameashiria baadhi ya maendeleo ya Iran na kusema: "Jamhuri ya Kiislamu iko tayari kuisaidia Saudi Arabia katika maeneo haya." 

Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu amesisitiza kuwa: Ni bora zaidi kwa ndugu wa eneo hili kushirikiana na kusaidiana badala ya kutegemea wengine.

Katika kikao hicho ambacho kimehudhuriwa pia na Mkuu wa Majeshi ya Iran Meja Jenerali Bagheri, Bwana Khalid bin Salman Waziri wa Ulinzi wa Saudi Arabia ameeleza kufurahishwa sana na kikao hicho na kusema: "Nimekuja Tehran nikiwa na ajenda ya kupanua uhusiano na ushirikiano na Iran katika nyanja zote, na tunatumai kuwa mazungumzo haya yenye kujenga yaliyofanyika yatajenga uhusiano imara zaidi kati ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Saudi Arabia.

342/

Your Comment

You are replying to: .
captcha